CALLIE, KIWAVI CHA KRISMASI
Hapo zamani za kale, katika mahali iitwayo Bethlehem, paliishi kiwaviaitwaye Callie.
Alikuwa kiwavi mzuri ambaye alijaribu kila awezalo kuepuka matata.
Hii ilikuwa ngumu hata hivyo, kwa kuwa mara nyingi alifanya maamuzi potovu.
Alikuwa kiwavi mzuri ambaye alijaribu kila awezalo kuepuka matata.
Hii ilikuwa ngumu hata hivyo, kwa kuwa mara nyingi alifanya maamuzi potovu.
Siku moja wakati alipokua akitafuta chakula cha kula, kiwavi huyo mdogoaliamua kukwea mlima. Alipofika juu, aliona kuwa kulikuwa na pango kubwalililozungukwa na miamba mengi. Callie alishikwa na msisimko wa kuchunguza. Hakuwa na uhakika kama ni wazo zuri kukwea ndani ya pangolenye giza, lakini aliamua kuingia hata hivyo.
Mara alipokuwa ndani ya pango, Callie alianza kuhisi baridi na upweke.Alishikwa na woga kwa sababu kamwe hakuwa amewahi kuingia pahali penyegiza na upweke hapo mbeleni. Kw haraka, aliamua kugeuka na kurudi. Kwa bahati mbaya, kiwavi huyo mdogo akaanguka chini kwa baadhi ya miamba nahakuweza kukumbuka njia ya kutoka nje. Je, alikuwa amegeuka kushoto au kulia? Callie hakujua!
Baada ya kupotea katika pango kwa muda uliloonekena kama mrefu sana,Callie alidhani kamwe hakuwa na uwezo wa kupata njia. Alikuwa amepoteakatika giza na akasema moyoni mwake, "Najuta kuingia pango kama hili la kutisha". Callie alihofu kwa sababu hakujua la kufanya.
Alikuwa karibu kupoteza matumaini kwa kuwa Callie alidhani hakuna mtuambaye angempata. Wakati huo huo, alisikia sauti ya punda, ng'ombe na kondoo. Sauti hizi zilimfanya afurahi kwa kuwa alihisi hayuko peke yake.
Ilikuwa msimu wa baridi na upepo mwingi Bethlehem, kwa hivyo wachungajiwaliamua kuleta wanyama ndani ya pango kulala. Mara baada ya wanaume hao kuingia wakiwa na mishumaa yao, Callie aliweza kuona kuwa pango ilikuwa kubwa sana. Katika chumba kubwa, wanaume hao waliweka nje boriti ya majanikwa ajili ya mifugo kupata malazi joto. Kama wanyama wengine, Kiwavi huyo alikuwa na usingizi mwingi baada ya siku ndefu. Kwa muda mfupi kila mtu alikuwa amelala.
Asubuhi wachungaji waliwaamsha mifugo na kwa haraka wakaondoka pangoni.Callie alipoamka, walikuwa tayari wamekwenda. Mifugo na wachungaji wa waliondoka mapema ili kufurahia joto ya jua la asubuhi. "Nitafanya nini sasa?",Callie akasema. Alihisi kama angeishi maisha yake yote ndani ya eneo hili.
Baada ya muda wachungaji wakarudi kwa ajili ya malazi ya wanyama wao kutokana na usiku ya majira ya baridi. Callie alihisi vyema kwamba kulikuwa na watu wengine katika pango pamoja naye, lakini alilia akijua kwamba kamwe hakuwa na uwezo wa kuondoka pango hilo kubwa. Hata kama mifugo badowalikuwa hapo, miguu yake ilikuwa fupi mno kwa ajili ya kufuata watu na wanyama kutoka giza hio.
Mara alipokuwa akijihurumia, kitu tofauti kilifanyika. Mtu mmoja aitwaye Yusufu aliingia pangoni. Alianza kuandaa kitanda cha majani, lakini si kwa ajili ya mnyama. Kitanda Hiki kilikuwa cha mke wake, Maria, ambaye alihitaji ili aweze kuzaa mtoto wake.
Kiwavi huyo alitazama kwa makini huku Maria akimshika mtoto wake mchanga wa kiume aliyeitwa Yesu. Mtoto huyo alikuwa amejazwa mwanga na upendo.Callie alipomwangalia Yesu,aliona kwamba hakua mpweke na mwenye hofu jinsi yeye alivyokuwa.
Usiku huo huo, wachungaji wengine waliingia pangoni na kuanza kuimbanyimbo kwa ajili ya mtoto Yesu. Pango iliyokuwa na giza mbeleni, sasa ikajazwa na mwanga iliyowafanya kila mtu kuihisi amani na furaha. Mara watu watatu wenye busara, ambao walikuwa wakifuatilia nyota yenye mwangaza zaidii,walikuja kutoa zawadi zao za Krismasi kwa mtoto Yesu. Wakampa dhahabu, ubani na manemane.
Callie alijawa na mshangao na heshima kwa mtoto huyu ambaye aliwafurahisha sana wale wote ambao walikuja kumtembelea. Hata hivyo alisikitika kwamba hakuwa na zawadi ya kumpa mtoto Yesu. Aliwaza, "Mimi ni kiwavi mpweke aliyepotea ndani ya pango hili, ni zawadi ipi naweza kutoa kwa ajili ya mtoto huyu ambaye ametupa mwanga wake?" Aliwaza na akawaza na akawaza zaidi.
"Ninajua!" Callie alisema. Alikuwa na msisimko kwasababu ya zawadiangeweza kutoa kwa Yesu. Aliamua kujifunga mwenyewe katika karatasi la zawadi ya krismasi. Kwa makini alifanya kifukofuko naye alivikwa ndani yamfuko. Wakati huo wote, Callie aliweza tu kufikiri kuhusu jinsi alitaka kutoazawadi yake kwa Yesu.
Baada ya kipindi kifupi, Callie alitoka nje ya kifukofuko hicho. Hapo ndipo aligundua muujiza wa Krismasi. Tena hakuwa kiwavi mpweke ndani ya pango. Alikuwa kiumbe kipya, kipepeo mwenye mabawa mazuri zaidi yenye umbo la moyo umbo.
Huku Callie akiruka kutoka gizani na kwa mwanga, tabasamu ilikuwa kwenyeuso wake. Alijua kwamba alifanya uamuzi mzuri na kwamba Yesu alikuwa na furaha kwa zawadi yake. Kila mara kipepeo anapoonekana akiruka katika hewa, tunakumbushwa tutoa mioyo yetu kwa Yesu.
Mwisho